Burudani

Wimbo utakaouzidi ‘Freedom’ utapata zawadi ya shilingi milioni tano – Sugu

Baada ya wimbo wa ‘Freedom’ kufanya vizuri kwenye media mbalimbali, Sugu anajipanga kuandaa shindano litakaloshindanisha wimbo utakaouzidi wimbo huo.

Sugu

Siku kadhaa zilizopita baada ya Sugu kuachia video ya wimbo wa ‘Freedom’ ulizua taharuki baada Mr Blue kulalamika kuwa Sugu kamuibia wimbo wake kabla ya uongozi wa studio ya MJ Record ambapo wimbo huo ulitayarishwa kuliweka sawa tatizo hilo.

Akizungumza kwenye kipindi cha FNL, kinachoruka kupitia EATV, Sugu amesema ‘tutaandaa shindalo la kushindanisha nyimbo itakayoizidi wimbo wa ‘Freedom’.

“Tumeshaongea na media moja ambayo tutapeleka wimbo wa ‘Freedom’ ambao wasanii wanaotaka watarekodi wimbo wataupeleka hapo. Kutakuwa na majaji kwenye shindano hilo watakaochagua nyimbo kumi bora na baadaye kupata nyimbo moja. Mshindi kwenye shindano hilo atapata shilingi milioni tano,” aliongezea.

Sugu amesema kwenye shindano hilo halitabagua msanii yeyote kila mtu anaruhusiwa hata awe Mr Blue.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents