Burudani

Nyota Ndogo: Unaweza kutunga nyimbo ukailia hela hata miaka 20

Kuna wasanii wengi ambao mpaka leo wanaendelea kunufaika kupitia kazi zao ambazo walizifanya miaka mingi iliyopita. Na kuna wengine ambao walitangulia mbele za haki lakini ndugu zao bado wanaendelea kufaidi matunda ya kazi zao.

nyota-ndogo-baraka-fm

Msanii wa Kenya, Nyota Ndogo amesimulia jinsi hit song yake ‘Watu Na Viatu’ inavyoendelea kumpa maisha hadi sasa licha ya kuwa ni wimbo ambao ni nadra sana kuusikia hata kwenye radio kwa kipindi hiki.

Kupitia Instagram Nyota Ndogo ameandika;

“Nimepata simu kutoka kwa mheshimiwa.ilikua hivi.HALLO HABARI YAKO MAMA NIKASEMA MZURI.MIMI NI FULANI DUH NIKASHTUKA.NIMEKUPIGIA NIMEAMBIWA HII NUMBER NI YA MTU ALIIMBA ILE NYIMBO YA WATU NA VIATU.NIKASEMA NDIO.AKASEMA HIO NYIMBO NINZURI SANA KISHA AKACHEKA.ALAFU AKASEMA NATAKA NIKUPE KAZI KWASABABU YA HIO NYIMBO UNATAKA PESA NGAPI?……yani anataka nikaimbe watu na viatu pekeake.unaweza kutunga nyimbo ukailia hela hata miaka ishirini.nyimbo ikasikizwa na watoto na watu wazima.nyimbo ikafatiliwa mpaka na waheshimiwa na wakakupa kheshma pia.tunasema SHUKRAN KWA MWENYEZI MUNGU.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents