Michezo

Nyota watano wa Yanga wabaki Dar

Timu ya Wananchi, Vijana wa Jangwani, Mabingwa wa Kihistoria Ligi Kuu Tanzania Bara na Mabingwa watetezi wa Michuano ya Mapinduzi Cup, Young Africans wametua katika visiwa vya marashi ya karafuu Zanzibar tayari kuanza kibarua chao cha kuutetea Ubingwa wao walioupata mwaka jana.

Yanga wametua Zanzibar mchana wa leo bila kuwepo kwa nyota wao watano ambao ni Dickson Job, Fiston Mayele, Feisal Salum, Jesus Moloko na Farid Mussa.

Vijana hao wa Jangwani hapo kesho Jumatano ya Januari 5, 2022 wanatarajia kushuka uwanjani katika mchezo wao wa kwanza kukabiliana na timu ya Taifa Jang’ombe.

Hata hivyo Yanga imeondoka na wachezaji wake ambao wamesajiliwa katika dirisha hili la usajili akiwemo kijana Denis Nkane aliyetokea Biashara United ya Mara.

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents