Michezo

Olimpiki: Brazil washinda medali ya dhahabu soka, Semenya aitoa kimasomaso SA

Neymar alimwagika machozi ya furaha baada ya kuisaidia Brazil ishinde medali ya dhahabu ya soka kwa mikwaju 5-4 dhidi ya Ujerumani, baada ya timu hizo kutoka suluhu kufuatia muda wa nyongeza, Jumamosi.

37720FE000000578-3750855-image-a-63_1471738393733

Brazil imewahi kupoteza kwenye fainali za Olimpiki mara tatu kabla, 1984, 1988 na 2012 – lakini hatimaye wamewapa furaha mashabiki wa mchezo huo waliohudhuria kwenye uwanja wa Maracana.

Neymar ndiye aliyefunga bao la kwanza katika dakika ya 22 kwa free kick kali lakini Ujerumani ikasawazisha kupitia nahodha, Maximilian Meyer.

Ushindi wa Brazil ni kisasi dhidi ya Ujerumani iliyowadhalilisha kwenye kombe la dunia mwaka 2014 kwa kuwafunga mabao 7-1.

Kwa upande wa Afrika Kusini, mkimbiaji Caster Semenya amewatoa kimasomaso kwa kushinda mbio za mita 800 na kushinda medali ya dhahabu.

bee5800101b4442bb86e27a69a69ec2a

Medali hiyo ya Semenya imeifanya SA iondoke na medali 10 kwenye michuano hiyo. Pia baada ya ushindi huo, Semenya alithibitisha kwa mara ya kwanza kuwa alimuoa mwanamke mwenzake, Violet Raseboya.

“Of course I’m happy. That’s what happens when you get married.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents