Habari

OSHA yaagwiza kupanua wigo programu za wajasiriamali wadogo

Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA)umegizwa kupanua wigo wa programu atamizi za wajasiriamali wadogo ili waweze kuyafikia makundimengi zaidi katika sekta zote za uzalishaji mali nchini.

Maagizo hayo yametolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi yaWaziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako, kupitia hotuba yakeiliyowasilishwa kwa niaba yake na Mwenyekiti wa Bodiya Usimamizi ya OSHA, Dkt. Adelhelm James Meru katika kikao cha Tano (5) cha Baraza la Nne (4) la wafanyakazi wa OSHA kilichofanyika jijini Arusha.

Agenda kuu ya kikao hicho ilikuwa ni kutathmini utendajikazi wa Taasisi hiyo kwa mwaka wa fedha uliopita(2021/22) pamoja na nusu ya kwanza ya mwaka wafedha 2022/2023.

“Ninawaagiza kupanua zaidi wigo wa programu atamiziya wajasiriamali (SMEs Incubation Programme) ilimuweze kuyafikia makundi mengi zaidi ya wajasiriamaliwadogo katika sekta zote kiuchumi. Tukifanya hivyo, tutakuwa tumeisadia sana nchi yetu kwani sekta isiyorasmi yenye makundi mengi ya wajasiriamali wadogondiyo inayoajiri idadi kubwa ya Watanzania,amesemaDkt.Meru.

Kwa mujibu wa taaarifa ya utekelezaji majukumu yaTaasisi ya OSHA kwa mwaka wa fedha uliopita(2021/2022), OSHA iliwafikia wachimbaji wa madini nawajasiriamali wadogo 11,204 zaidi ya lengo lawajasiriamali 10,000. Hivyo, Waziri mwenye dhamanaya Masuala ya Kazi kuwataka kuweka malengo yakufikia idadi kubwa zaidi katika kipindi kijacho.

Aidha, Dkt. Meru amewataka wafanyakazi wote waOSHA kufanya kazi kwa bidii na kuongeza ubunifu zaidiili waweze kuongeza tija katika Taasisi na Taifa kwaujumla.

Natambua kwamba Taasisi hii yenye dhamana yakulinda nguvukazi ya Taifa letu bado ina kazi kubwa yakufanya kwani maeneo ya kazi hapa nchini ni mengi nayanazidi kuongezeka kila siku hivyo tunahitajikakujituma zaidi na kuwekeza zaidi katika miundombinuna rasilimali muhimu zitakazotuwezesha kufikishahuduma hizi muhimu za masuala ya Usalama na Afya kwa watanzania woteamesema Dkt. Meru.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, amesema kuwa katika mwaka wa fedha2021/22 Taasisi anayoiongoza ilitekeleza majukumuyake kikamilifu na hivyo kuvuka baadhi ya malengoiliyojiwekea katika mwaka huo wa fedha.

Tulifanikiwa kusajili maeneo ya kazi 7,260 ukilinganishana lengo la kusajili maeneo ya kazi 7,000 na hivyokufikia asilimia 103.7. Mafanikio mengine ni pamoja nakufanya kaguzi 217,102 ukilinganisha na kaguzi200,000 zilizopangwa kufanyika, kupima afya jumla yawafanyakazi 252,733 zaidi ya lengo la kupimawafanyakazi 250,000, kutoa mafunzo kwa maafisa14,661 ikilinganishwa na maafisa 10,000 waliolengwa.amesema Mtendaji Mkuu huyo wa OSHA.

Nae Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu, wakatiakifunga kikao hicho cha tano cha baraza la nne la wafanyakazi wa OSHA, amewataka watumishi wotekuendelea kuchapa kazi huku akiwahakikishia kuwaataendelea kushirkiana na viongozi wa Taasisi hiyokutatua changamoto wanazokumbana nazo katikautekelezaji wa majukumu yao.

Nitumie fursa hii kuwahakikishia kwamba sisi viongoziwenu tupo pamoja nanyi na tutajitahidi kwa kadriinavyowezekana kusaidia kutatua changamotozilizoainishwa ili kuiwezesha Taasisi yenu yenyedhamana kubwa ya kulinda nguvukazi ya Taifa kuwezakufanikisha malengo yake. Hivyo, nisisitize kila mmojawetu kuchapakazi pamoja na kuzingatia weledi namaadili ya utumishi umma kwa maslahi mapana yaOSHA na Tanzania kwa ujumla,amesema Prof. Jamal Katundu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents