Habari

Papa amtimua kiongozi wa dini kwa kusambaza kondomu

Kiongozi wa kanisa katoliki anayewasaidia raia wa Malta amejiuzulu kufuatia mgogoro na Vatican kuhusu mpango wa kusambaza mipira ya kondomu kulingana na kanisa hilo.

Mathew Festing mwenye umri wa miaka 67 alijiuzulu baada ya papa Francis kumtaka kufanya hivyo katika mkutano siku ya Alhamisi. Hatua hiyo inafuatia ufichuzi kwamba tawi la hisani la kanisa hilo huko Malta lilisambaza maelfu ya mipira ya kondomu katika taifa la Myanmar.

Papa Francis alimtaka ajiuzulu na alikubali kwa kuwa kanisa hilo linakataza utumizi wa mipira ya kondomu.

Tawi hilo la Malta lina uwezo mkubwa kama ule wa taifa zima. Hutoa pasipoti, stempu na leseni na pia lina uhusiano wa kidiplomasia na mataifa 106 ,ikiwemo Vatican.

BY: Emmy Mwaipopo

Chanzo: BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents