Michezo

Patrice Evra ampiga shabiki ‘karatee’ apewa kadi ya historia (Picha)

Beki wa zamani wa klabu ya Manchester United, Patrice Evra jana usiku ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya soka kupewa kadi nyekundu hata kabla ya kuanza kwa mechi ya Europa league.

Beki Patrice Evra ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kulambwa kadi nyekundu hata kabla ya mechi kuanza katika michuano ya Eurpa League.

Evra ambaye kwa sasa anacheza katika klabu ya Marseille hapo jana usiku alishuka dimbani katika usiku wa michuano ya Eurpa League kukipiga dhidi ya Vitoria de Guimaraes ghafla ameonekana akimrukia shabiki na kuanza kumpiga.

Evra alishindwa kuvumilia maneno aliyokuwa akiambiwa na shabiki wa timu yake ya Olympique Marseille kabla ya mchezo kuanza wakati akipasha misuli ilikujiandaa na mchezo huo ambao ulimalizika kwa kufungwa bao 1-0 na Vitoria Guamares.

Zifuatazo ni picha za matukio

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents