Burudani

Picha: Dogo Janja achora Tattoo ya Irene Uwoya kwenye kwapa

Tangu walipofunga ndoa imekuwa vigumu kuwakosa kwenye headlines za kiburudani Bongo, time hii Dogo Janja amechora tattoo ya Irene Uwoya kwenye kwapa.

Kuchora tattoo inaweza isiwe ishu, stori ni eneo ambalo tattoo yenyewe imechorwa si kawaida. Kupitia Instagram Dogo Janja ameweka picha hiyo na kuandika; I made this infinity Promise for you @ireneuwoya8 #NoMoreDrama🌹.

Utakumbuka hatua hiyo ni baada ya Irene Uwoya kufanya kitu kama hicho miezi kadhaa iliyopitia ambapo Dogo Janja alimtaka kuchora nyingine.

Dogo Janja na Irene Uwoya waliripotiwa kufunga ndoa November 25, 2017, hata hivyo ni vigumu kutaja tarehe kamili kutokana na namna walivyoliweka suala hilo hasa kwa upande wa vyombo vya habari na mitandao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents