Burudani

Picha : Huu ndio mjengo wa Jay Z na Beyonce wanaoishi na mapacha wao

Baada ya kujifungua mapacha na kukaa nao kwa muda wa wiki moja na nusu katika kituo cha afya cha UCLA, wakiwa chini ya uangalizi maalumu wa madaktari, hatimaye Beyonce na mapacha wake waruhusiwa kutoka hospitalini hapo na kuhamia katika mjengo wao mpya.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, watoto hao ambao wamezaliwa njiti maweruhusiwa kutoka na wameungana na dada yao Blue Ivy pamoja na familia yao katika jumba la kifahari la kukodi lililopo Malibu Estate. Inadaiwa kuwa mjengo huo umewagharimu Jay Z na Queen Bey kiasi cha dola 400,000 ambapo wanatarajiwa kuishi hapo kwa muda wa mwezi mmoja.

Hizi ni baadhi ya picha za jumba hilo la kifahari.

Jay Z na Beyonce bado wapo katika utaratibu wa kutafuta nyumba nyingine ya kwao ya kuishi baada ya kutoka hapo, nyumba hiyo mpya inatafutwa katika maeneo ya Los Angles.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents