Habari

Picha: Kampeni ya Nipe Fagio yasherehekea Valentine’s Day kwa kusafisha fukwe za Msasani

Kampeni ya Nipe Fagio iliitumia weekend ya Valentine’s Day kusafisha fukwe za Msasani jijini Dar es Salaam.

Wiista, Kiche & Mswati
Wiista, Kiche na Mswati

“Siku hiyo ya Valentines tulikusanya magunia ya uchafu 112 kwa kushirikiana na wananchi wa Msasani wakiongozwa na mwenyekiti wao Mr. Seif Soud Seif kwa kushirikiana na Nipe Fagio pamoja na Archipelago Productions,” amesema Ben Kyambile aliyeshiriki pia kufanya usafi.

Yusuf kutoka Nipe Fagio
Yusuf kutoka Nipe Fagio

“Watu wengi sana walijitokeza kusaidia kusafisha beach hiyo na watu wengi hawajui thamani ya hiyo beach kwasababu hiyo ndio beach pekee public ukiachana na Coco beach. Ndio beach ya pili ukitoa Coco ambayo wananchi wanaruhusiwa kupumzika bila kulipia chochote. Zoezi hilo la usafi litakuwa linafanyika kila Jumamosi ya pili ya kila mwezi,” ameongeza.

Sarah Scott na Seif Soud (Mwenyekiti wa Msasani)
Sarah Scott na Seif Soud (Mwenyekiti wa Msasani)

“Shughuli hiyo ya usafi ilikuwa na lengo la kuamsha ushiriki kwenye usafi wa mazingira yetu na kukick off Takataka Bucket Challenge, na jana Wasanii Wiista na Kiche wamejiandikisha kufanya challenge hiyo kwahiyo tutaona video zao mtandaoni siku za karibuni.”

Mwenyekiti akiokota uchafu na Wananchi

IMG_8329

IMG_8322

IMG_8294

IMG_8285

IMG_8225

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents