Picha: Maelfu ya waombolezaji wajitokeza kwa wingi katika uwanja wa FNB, Johannesburg, licha ya mvua inayoendelea kunyesha
Licha ya mvua inayoendelea kunyesha nchini Afrika Kusini toka asubuhi ya leo (December 10), maelfu ya watu tayari wamekusanyika katika uwanja wa mpira wa FNB wenye uwezo wa kuchukua watu 95,000 ulioko Soweto, katika jiji la Johannesburg, Afrika Kusini, tayari kwa shughuli maalum ya kihistoria ya kumuaga aliyekuwa Rais wa taifa hilo Nelson Mandela, shughuli inayoendelea hivi sasa.
Marais mbalimbali zaidi ya 100 akiwemo Rais Jakaya kikwete, Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Uhuru Kenyatta wa Kenya tayari wamewasili. Wengine ni Marais wa Marekani Barrack Obama, Bill Clinton na George W. Bush, na marais mbalimbali wa dunia wamewasili Afrika Kusini tayari kwa shughuli hiyo muhimu na ya kihistoria ambayo inaonekana moja kwa moja na dunia nzima (muda huu 12:53 hrs) kupitia kituo kikubwa cha TV cha BBC.
Rais Kikwete katika uwanja wa ndege wa Waterkloof Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria
Rais wa Uganda Yoweri Museveni akiwasili Afrika Kusini
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akiwasili Afrika Kusini
Obama na First Lady Michelle baada ya kushuka kwenye Air Force One Afrika Kusini
George W. Bush na mkewe Laura, pamoja na Hillary Clinton
David Cameron akiwa tayari uwanja wa FNB
Rais wa Zimbambwe Robert Mugabe na mkwewe Grace Mugabe
Rais wa Equatorial Guinea, Teodoro Obiang Nguema Mbasogo
Malawi’s President Joyce Banda
Pakistani President, Mamnoon Hussain
Mmoja wa waombolezaji asubuhi ya leo akielekea uwanjani
PICHA: MAIL ONLINE, PICHA YA KIKWETE: JESTINA GEORGE