Habari

Picha: Mashindano ya Miss Tanzania 2016 yazinduliwa

Mashindano ya Miss Tanzania yaliyowahi kufungiwa kwa miaka miwili kufuatia skendo ya Sitti Mtemvu yamezinduliwa tena.

unnamed (3)
Mkurugenzi wa kampuni ya Lino International Agency, Hashin Lundenga akiongea kwenye uzinduzi huo

Hafla ya uzinduzi wa msimu mpya wa mashindano hayo ilifanyika kwenye hoteli ya Ramada Resort iliyopo Kunduchi, Dar es Salaam.

unnamed
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto) akifurahi jambo na mmoja wa wajumbe wa kamati ya Miss Tanzania. Wengine ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa, Geogrey Mngereza na Lundenga

Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye. Wengine waliohudhuria ni pamoja na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa, Geogrey Mngereza, warembo waliowahi kushika taji la Miss Tanzania miaka iliyopita na mawakala wanaoandaa mashindano ya Miss Tanzania katika ngazi mbalimbali hapa nchini.

unnamed (6)
Kutoka kushoto ni Miss Tanzania 1998, Basila Mwanukuzi, Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu, Miss Tanzania 2008, Nasreen Kareem pamoja na Miss Tanzania 2014/2015, Lilian Kamazima wakipozi katika picha ya pamoja kwenye uzinduzi wa Msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016

unnamed (5)
Linah akitumbuiza kwenye hafla hiyo

unnamed (2)
Miss Tanzania 2014/2015, Lilian Kamazima na Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu

Picha: Mo Dewji Blog

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents