Michezo

Kauli kuhusu ushoga yamfanya Pacquiao apigwe marufuku kuingia kwenye mall maarufu ya LA

Baada ya kampuni ya Nike kusitisha mkataba na bondia wa Ufilipino, Manny Pacquiao kufuatia kauli yake kuwa mashoga ni wabaya zaidi ya wanyama, mall maarufu ya jijini Los Angeles, Grove imempiga marukufu.

75451b114b3faf3c0906096c93bcb798

Mmiliki wa mall hiyo, Rick Caruso amedai kuwa uamuzi huo umechukuliwa kwakuwa watu wengi wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja ni wateja wa mara kwa mara wa mall hiyo na kwamba wana haki ya kujisikia vibaya.

“Hivyo Manny Pacquiao hakaribishwi tena,” alisema.

Kauli hiyo iliyowakasilisha watu wengi wanaojihusisha na mapenzi hayo ilimfanya aombe radhi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents