Habari

Picha: Mchungaji awaambiwa waumini kula majani ili kuwa karibu na Mungu

Umaskini, magonjwa na matatizo mengine yanayowakabili binadamu, yamewafanya waamini kila kitu wanachoambiwa na viongozi wao wa dini kama njia ya kuyaondoa.

Muumini akila majani ili kuwa karibu na Mungu
Muumini akila majani ili kuwa karibu na Mungu

Mchungaji wa nchini Afrika Kusini amewafanya waumini wake wale majani kama mbuzi ‘eti’ kuwa karibu na Mungu.

Mwanamke mmoja alidai kuwa kula majani kulimponya koo lake
Mwanamke mmoja alidai kuwa kula majani kulimponya koo lake

Kwa maelekezo ya Pastor Lesego Daniel wa Rabboni Centre Ministries, mamia ya wafuasi wake walijimwaga kwenye uwanja nje ya kanisa lake kula majani huko Garankuwa, Kaskazini mwa Pretoria baada ya kuambiwa kuwa kwa kufanya hivyo wanakuwa karibu na Mungu.

Waumini wakiwa wamelala nje ya kanisa kula majani kama walivyoagizwa na mchungaji wao
Waumini wakiwa wamelala nje ya kanisa kula majani kama walivyoagizwa na mchungaji wao

Mbinu hiyo yenye utata imekosolewa na watu wengi huku yeye akisema kuwa binadamu wanaweza kula chochote na wasidhurike. “Ndio tunakula majani na tunajivunia sababu inaonesha kuwa kwa nguvu ya Mungu, tunaweza kufanya lolote,” Rosemary Phetha aliliambia gazeti la Afrika Kusini la Times Live.

Kula majani kama mbuzi

Doreen Kgatle, 27, alipata kiharusi miaka miwili iliyopita anasema: Sikuweza kutembea lakini baada ya kula majani kama mchungaji alivyoagiza, nilianza kupata nguvu na saa moja baadaye niliweza kutembea tena.”

Picha zinazoonesha waumini mbalimbali wakila majani huku mchungaji huyu akiwakanyaga zimeleta mjadala mkubwa.

article-2537053-1A8B310100000578-989_306x423
Matokeo baada ya kula majani, kuumbwa tumbo na kutapika

article-2537053-1A8B320400000578-643_306x423

Baada ya kula majani kilichofuata kilikuwa hiki

Times Live limeandika kuwa kwenye misa hiyo ya watu takriban 1,000 Daniel alisikika akisema ‘lala’ na watu sita wakalala usingizi. Aliwaagiza watu wengine kuwapiga vibao na kuwatikisa lakini watu hao walienda kulala bila kujitambua hadi pale alipowaagiza waamke.

1551669_711412385544134_1720454493_n

1497616_711412412210798_250937811_n

1507770_711412475544125_940043098_n

1526340_711413345544038_1450047438_n
‘Unaweza kuwaacha hivi kwa miezi sita. Naipenda hii. Sipendi kuboreka. Unaweza hata kuwafanya polisi wasinzie pindi wanapokuja kukukamata,” alisema.

Bonyeza hapa kwenda kwenye ukurasa wa Facebook wa kanisa hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents