Picha: Ronda Rousey asema ‘nitarejea’, ni baada ya kupigwa kwa KO ya aibu na Holly Holm
Bondia Ronda Rousey amezungumza kwa mara ya kwanza baada ya kushindwa kwa knock-out Jumapili ya jana na Holly Holm.
Teke la Holly Holm lililomdondosha Ronda Rousey chini
Rousey alishindwa vibaya baada ya kuangushwa kwa teke kali la Holm kwenye raundi ya pili ya mchezo huo wa UFC uliovunja rekodi kwa kushuhudiwa na 56,214 huko Melbourne, Australia.
Hilo ni pambano la kwanza kwa bondia huyo kushindwa.
Baada ya pambano hilo bondia huyo alipelekwa kwenye hospitali ya mjini humo na kushindwa kuhudhuria mkutano na waandishi wa habari.
Kupitia Instagram Rousey aliandika: Nilitaka kumshukuru kila mmoja kwa upendo na support,” alisema Rousey.
“Nashukuru kwa wasiwasi wenu kuhusu afya yangu lakini niko salama. Kama nilivyosema mwanzo, ntapumzika kwa muda kiasi, lakini nitarejea.”
Rais wa UFC Dana White amedai kuwa uwezekano wa kuwepo mechi ya pili kati ya mabondia hao ni mkubwa.