Habari

Picha: Tigo yatangaza washindi wa shindano la Tigo Digital Change Maker

Kwa awamu nyingine, Tigo wamewatangaza washindi wa shindano la Tigo Digital Change maker linalowatafuta washindi wawili na kuwazawadia kiasi cha dola $20,000, kila mmoja na usimamizi wa kitaalamu kwenye mchakato huo na ushauri kutoka Tigo na kampuni mwenza ya Reach for Change.


Meneja wa Tigo Tanzania Diego Gutierrez

Alhamis hii, Tigo imetangaza washindi wa Tigo Digital Change Makers ambapo ni Nancy Sumari kupitia mradi wake wa Jenga Hub na Sophia Mbega kupitia kikundi cha VicobaApp.


Meneja wa huduma za jamii, Woinde Shishael

Washindi hao wametangazwa mapema leo katika makao makuu ya Tigo yaliyopo Makumbusho jijini Dar es Salaam, sambamba na kuhudhuriwa na waandishi wa habari pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo.


Sophia Mbega huyu ni mshindi wa kwanza katika shindano hilo

Kwa upande wa Sophia Mbega, amesema kwenye Vicoba walikuwa wanatoa msaada wa kifedha kwa vikundi vya vicoba sambamba na kutoa ahadi ya kushirikiana na kuishukuru Tigo na Reach for Change.

Naye Nancy Sumari kupitia Jenga Hub, amekuwa akiwasaidia watoto wadogo kiteknolojia. Aidha lengo lake ni kuwasaidia watoto shuleni kwenye ya hesabu na Kiingereza, kusoma na kuandika. Amewashukuru Tigo na Reach for change na kudai ana uhakika wa kuwafikia watu wengi zaidi Tanzania huku akihakikisha hakuna mtoto atakayekuwa nyuma katika gurudumu la TEHAMA.

Hizi ni baadhi ya picha:


Nancy Sumari huyu ni mshindi namba mbili katika shindano hilo


Hapa washindi wakiwa katika picha ya pamoja

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents