Bongo Movie

Picha : Uzinduzi wa filamu mpya ya ‘Bantu’ ulivyobamba

Sekta ya filamu inazidi kukuwa kwa wasanii kuonyesha uwezo wao sanjari na kuibua vipaji vipya katika soko, ili kuleta ushindani na kuzalishaa filamu zanye ubora.

Hayo yamedhihirika katika uzinduzi wa filamu mpya ya ‘Bantu’ uliofanyika Ijumaa ya wiki hii maeneo ya Escape One-Mikocheni, ambapo macho ya wapenda burudani wameitazama filamu hiyo inayokwenda sambamba na maisha ya vijana wengi nchini.

Filamu ya ‘Bantu’ ni filamu inayomuhusu kijana mmoja aitwaye Bantu ambaye amekuwa akishiriki mahusiano ya kimapenzi na wanawake tofauti tofauti , jambo linalompelekea kuja kutapa ugonjwa wa Ukimwi bila kujua na kujikuta akitaka kuingia katika mahusiano na binti mrembo ambaye yeye alipata maambukizi ya Ukimwi toka utotoni. Bantu anajikuta akimpenda mrembo huyo na kutaka kuachana na maisha yake ya mwanzo, ila mtihani ni pale anapotakiwa kwenda kupima Ukimwi kabla ya tendo la ngono.

 

Na Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents