Habari

Picha: Wabunge walivyopiga mechi ya Mpira, Simba na Yanga style!

Mamia kwa maelfu ya wakazi wa jiji la Dar-Es-Salaam na vitongoji vyake walifurika katika uwanja mkuu wa taifa kushuhudia tamasha la burudani mbali mbali za kimuziki, Ndondi pamoja na mpira wa miguu uliohusisha wabunge wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania wanaoshabikia timu za Yanga na Simba, Bongo Flava dhidi ya Bongo Muvi, mpambano wa Wema na Jackline Wolper na mwisho kabisa Ngumi kati ya bondia Japhet Kaseba na Francis Cheka.

Tamasha hilo lililoandaliwa kwa pamoja baina ya Kampuni ya Global Publishers kupitia kitengo chake cha Burudani kwa kutumia platform yao ya ukumbi wa burudani Dar Live, pamoja na mfuko wa elimu na kulipa jina tukio hilo kuwa la Tamasha La Matumaini lilikuwa mahususi kuchangia mfuko wa elimu kwa wasichana katika ujenzi wa mabweni katika shule ya Kongwa mkoani Dodoma.

Watu wa marika mbali mbali walihudhuria tamasha hilo ambalo lilianza rasmi majira ya saa tisa kamili ambapo timu ya Bongo Fleva ilipambana na timu ya Bongo Muvi na timu ya Bongo Fleva kuondoka na ushindi wa goli moja dhidi ya Bongo Fleva katika pambano lililokuwa la kuvutia na vituko pamoja na vibweka kibao. Alikuwa… ambaye aliwainua mashabiki wa Bongo Muvi baada ya kufunga goli katika dakika ya 64 ya kipindi cha pili.

Baada ya hapo burudani ya mpira haikuishia hapo, ilikuwa ni zamu ya timu za Simba na yanga kwa upande wa wabunge ambapo timu ya samba iliongozwa nao waziri wa Tamisemi elimu Mheshimiwa Kassim Majaliwa, waziri wa zamani wa nishati na madini William Ngeleja, Iddi Azzan, Joshua Nassari, Adam Malima pamoja na Zitto Kabwe.

Upande wa pili wa timu ya Yanga kulikuwepo na Deo Filikunjombe, Peter Mwesigwa, Mpira huo ulikuwa ni burudani tosha kwani ulikuwa na hisia za kikweli kweli za samba na yanga baada ya timu zote kuongozwa na mabenchi ya ufundi ya timu zenyewe haswa haswa timu ya wabunge wa Yanga ambao kwenye benchi alikuwepo kocha mpya wa sasa mbelgiji pamoja naye Salvatory Edward.

Aidha mpira huo uliisha kwa timu ya wabunge wa Simba kushinda goli 3 kwa 2 kwa njia ya penati baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana katika lisaa limoja waliocheza mpambano huo. Jambo la kushangaza ambalo ni mbunge Joshua Nassari ambaye mwanzo katika dakika 60 za mchezo huo alicheza ndani kabla ya kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Peter Mwesiga lakini baada ya kipa namba moja wa timu ya wabunge wa Simba Idd azzan kutoka baada ya kupata majeraha Joshua Nassari alikwenda golini na kufanya kazi nzuri ya kudaka mipira kama kipa wa kweli kweli.

Shuhudia picha kama hivi mdau!

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents