Michezo

Picha: Wachezaji wa Everton wafanya mazoezi na ‘Albino United’ uwanja wa Uhuru

Mara baada ya kuwasili nchini Kikosi cha Everton kwaajili ya mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia baadhi ya wachezaji wa timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza akiwemo beki wao mpya Michael Keen wamefanya mazoezi na timu ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino United) katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.

Everton ambayo imewasili leo majira ya saa mbili asubuhi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere inatarajia kujitupa uwanjani kesho kuhitimisha michuano ya SportPesa Super Cup dhidi ya Bingwa, Gor Mahia.

Hata hivyo baada ya mazoezi hayo waliweza kutoa msaada wa vitu mbalimbali vya kimichezo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents