Burudani

Picha: Will Smith amkata mtoto wake nywele

Staa wa filamu nchini Marekani, Will Smith hataki mchezo kabisa na kazi. Ameamua kumkata mtoto wake nywele ili tu afanye movie inavyotakiwa.

Will Smith amefanya uamuzi huo wa kumkata mtoto wake rasta Jaden Smith ambaye pia ni staa wa filamu Hollywood.

Jaden anajipanga kuigiza filamu ya ‘Life In A Year’ na ili kwenda sawa na uhusika wake alibidi akate nywele. Baada ya Will kuona kuwa dogo analeta ubishi aliamua kuzifyeka mwenyewe.


Muonekano mpya wa Jaden

Filamu ya Life In A Year ina kisa cha uhusiano wa kimapenzi kati ya Jaden na Cara Delevingne. Jaden anagundua mpenzi wake ana mwaka mmoja tu wa kuishi na anafanya analoweza kuhakikisha wanaishi kwa furaha na kufanya yote walioota kufanya. Filamu hiyo itaanza kutayarishwa Toronto, Canada.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents