Burudani

Picha: Young Dee atoa msaada vituo vya watoto yatima maandalizi ya BBM Tour Kahama

Msanii wa muziki Young Dee aka Rapa Paka katika kuelekea sherehe za Edi El Fitr Jumatatu hii ametoa msaada wa chakula pamoja na vifaa mbalimbali vya shule kwa vituo viwili vya watoto yatima vilivyopo Kahama ikiwa ni maandalizi ya show ya BBM Tour inayotorajiwa kufanya leo katika uwanja wa Taifa Kahama.

Young Dee akiwa na team yake.

Akizungumza wakati akikabidhi misaada hiyo, Young Dee alisema ameamua kushare kile kidogo alichonacho na watoto yatima na wao wajisikie vizuri katika kipindi hichi cha sikukuu.

“Kile kidogo nilichopata nimeona ni bora nishare na watu ambao mara nyingi wanasahaulika, sisi ndio watu ambao tunatakiwa kuwakumbuka na kuhakikisha tunawasaidia katika mambo kadhaa,” alisema Young Dee.

Rapa huyo aliweza kutoa mchele, sukari, mafuta, hela pamoja na madaftari. Angalia picha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents