Mitindo

Picha:’Area Code’ yaendesha mafunzo kwa Models wake

Kampuni wa Models pamoja na kusimamia wasanii ‘Area Code Entertainment’ Jumamosi hii katika ukumbi wa Maisha Basement jijini Dar imeendesha mafunzo ya siku moja kwa models wake, jinsi ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili.
Area Code wakiwa  wenye furaha
Area Code wakiwa wenye furaha

Mafunzo hayo ambayo yalipewa jina la ‘Meet, Greet and Inspire’ yaliendeshwa na mshindi wa tuzo ya mpiga picha bora wa Swahili Fashion 2015, Ousman Kazi pamoja na Mwanamitindo bora wa Swahili Fashion 2015, Upendo Mlay pamoja na wadau wengine wa Fashion.

Akizungumza na Bongo5 Jumamosi hii Mkurugenzi wa Area Code Entertainment, Nahuja Hatibu amesema aliona ni vema kuwapa mafunzo vijana wake kwa kuwa vijana wengi huingia kwenye fashion bila kujua changamoto zake.

“Meet, greet and inspire imekuja kwa sababu tuligundua watu wengi wanaingia kwenye tasnia ya fashion kichwa kichwa bila kujua changamoto zake, wanapata sana shida kwa sababu wanatakiwa kuhonga, lakini kupitia watu ambao tayari wamezipitia hizi changamoto naimani watu wangu watajifunza ,” alisema Hatibu

Aliongeza,”Haya mafunzo yataendelea tena kwa sababu kama vilivyokwambia hii kampuni inafanya mambo mengi sana, kwa hiyo usishangae wakati ujao tukawaleta wasanii ili kuwasaidia Models ambao wanataka kuwa wasanii. Kwa hiyo mwezi ujao tutakuwa tena hapa au sehemu ngingine kwa ajili ya mafunzo mengine,”

Pia kwa upande wa Mwanamitindo bora wa Swahili Fashion 2015, Upendo Mlay amewataka models kujiheshimu na kufanya kazi kwa bidii.

“Kikubwa ni kujiheshimu tu, unajua kama unafanya kazi kwa kujiheshimu hata watu serious watakutafuta na utafanya nao kazi. Lakini ukiwa ni mtu usiyoeleweka utapata shida sana kufanikiwa,”. alisema Upende.

Model wakisikiliza mafunzo kwa umakini
Model wakisikiliza mafunzo kwa umakini

Mwanamitindo bora wa mwaka wa Swahili, Upendo Mlay (kulia) akimkabidhi cheti za Model wa kampuni ya Area Code
Mwanamitindo bora wa mwaka wa Swahili, Upendo Mlay (kulia) akimkabidhi cheti za Model wa kampuni ya Area Code

Photographer Ousman Kazi (kulia) akimkabidhi cheti Model wa Area Code
Photographer Ousman Kazi (kulia) akimkabidhi cheti Model wa Area Code

Photographer Ousman Kazi akitoa mafunzo wa Models
Photographer Ousman Kazi akitoa mafunzo kwa Models

Team Area Code akiwa katika picha ya pamoja
Team Area Code akiwa katika picha ya pamoja

_K0A3999

_K0A4030

_K0A4033

_K0A4040

_K0A4046

_K0A4063

_K0A4075

_K0A4100

_K0A4102

_K0A4104

Area Code wakiwa  wenye furaha

IMG_0250

IMG_0251

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents