Habari

Picha/Video: Ziara ya Dkt Shein yafanikisha kuzindua miji ya kisasa Zanzibar

Katika kuhakikisha serikali ya awali ya saba kisiwani Zanzibar inatekeleza ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2015-2020 ya kuwapatia maisha bora wakazi wake Rais wa Serikali ya Mapinduzi, Dkt Ali Mohamed Shein ameweza kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya ujenzi wa makazi ya kisasa iliyopo Wilaya ya Magharibi B, katika Mkoa wa Mjini Magharibi.

Ujenzi huo ambao upo katika maeneo ya Nyamanzi na Fumbo, unatarajiwa kusaidia  kuweka makazi bora  kisiwani hapo na kutoa ajira kwa wazawa wa sehemu hiyo.  Vile vile Dkt Shein amezindua tawi jipya la Chama Mapinduzi ( CCM ) eneo la Bwelo, na kuwataka wanachama kutumia tawi hilo kwa manufaa ya chama chao.

Na Laila Sued na Salum Kaorata

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents