Burudani

Professor J alaani mauaji ya albino, atoa ushauri kwa serikali na wananchi

Msanii mkongwe wa Hip Hop, Professor Jay amelaani vikali matukio yanayoendelea ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi ‘albino’ huku akiitaka serekali pamoja na wananchi kuungana pamoja katika kuhakikisha wanakomesha matukio hayo.

profesa-Jay

Jay amesema hayo baada ya mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Baraka Cosmas Lusambo mwenye umri wa miaka 9 katika kitongoji cha Kikonde kata ya Kipeta wilaya ya Sumbawanga vijijini kukakwa kiganja cha mkono na watu wasiojulikana na kutokomea nacho.

Barakah Cosmas Lusambo
Barakah Cosmas Lusambo

Akizungumza na Bongo5 leo, Professor amesema anaunga mkono jitihada mbalimbali ili kukomesha ukatili huo huku akiandaa wimbo mpya wa kuelimisha jamii kuhusu vitendo hivyo.

“Huu ni unyama unyama uliokithiri na unapingwa na kila binadamu,” amesema. “Sisi kama wasanii tupo mstari wa mbele kupaza sauti zetu ili kujaribu kukomesha haya mambo. Pia tupo kwenye mpango wa kuandaa wimbo wa kuelimisha jamii kuhusu haya mambo. Naiunga mkono kampeni ya Mdimu, Inatosha na pia rais aliwahi kuzungumza na walemavu wa ngozi. Hizi zote ni jitihada za kuangalia jinsi gani tunakomesha mauaji ya ndugu zetu,” ameongeza rapper huyo aliyetangaza kugombea ubunge mwaka huu.

“Lakini hii haitoshi tunahitaji kufika katika maeneo ambayo haya matukio yanatokea mara kwa mara, kuongea nao pamoja na kuwaelimisha kuhusu kuepuka imani za kishirikina ambazo zinadaiwa kusababisha haya mambo. Kuelisha jamii na kuwaondoa hofu juu yao na kuwafichua watu wanaojihusisha na haya mambo kwa sababu hawa watu wanaofanya wapo katika mazingira tunayoishi. Kwahiyo tukishirikana kwa pamoja tunaweza tukafikia sehemu fulani.”

Katika hatua nyingine, Professor ameipongeza serikali kwa kuhukumu kunyongwa mpaka kufa kwa baadhi ya watu waliokutwa na tuhuma za kuhusika na mauaji wa walemavu wa ngozi.

“Nimefurahi sana kusikia hiyo adhabu lakini mimi naona kama serikali bado ina makucha zaidi. Inaweza ikafanya makubwa zaidi au kuongeza adhabu sijui mpaka wapi ili tu mtu akisikia ajue hii ni hatari sana.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents