“Sijaacha muziki baada ya kuoa”
Kila mshabiki wa muziki wa kizazi kipya aliamini kuwa msanii Soggy Doggy a.k.a Chief Rumanyika kuwa baada ya kuvuta jiko na muziki tena basi kutokana na kimya cha ajabu ambacho kimezuka hasa baada ya kutawazwa rasmi kuwa ni mume wa mtu.

unajua hainishangazi kusikia kutoka kwa watu kuwa Soggy amesimama masuala ya muziki mara baada ya kuoa, ndio maana ili kukata ngebe na vilimi limi vyao nimeamua kutoa ngoma mbili kwa mpigo na zite zikiwa na maana na kwa walengwa maalum alisema Soggy Bingo.
Msanii huyu ambaye kwa sasa ni meneja katika kituo maarufu cha redio mkoani Arusha Tripple A FM, hivi karibuni ametoa ngoma mbili kwa pamoja ambazo zinakwenda kwa majina ya ICU na My Baby’ ambazo zote nimelenga masuala yaliyo ya ukweli kabisa katika jamii inayotuzunguka.
Wimbo My Baby ni dedication kwa mke wangu mpendwa ambapo nimeongelea mambo mengi tu ya kumfanya ajisikie raha kuimbiwa na mumewe, na hii nyingine ICU’ ni maalum kwa wasanii ambao waliwahi kupata mafanikio katika sanaa wakacheza na sasa wako mahututi kisanaa na maisha yao kwa ujumla Soggy.
Huu ni ujio mpya wa Albam ya msanii huyu itakayokwenda kwa jina la Haina Kufoward’ na ngoma ambazo ameziachia zote zimefanyikia katiaka studio maarufu mkoani Arusha ijulikanayo kwa jina la Noise Mekah chini ya prodyuza DX.