Burudani

Queen Darleen aeleza anakuja na mtindo gani akiwa ndani ya WCB

Msanii mpya wa WCB, Queen Darleen ‘Queen wa WCB’ amefunguka na kusema kuwa akiwa ndani ya WCB atafanya muziki wa kila aina ilimradi mkono uende kinywani.
Queen wa WCB

Muimbaji huyo ambaye pia ni dada ya rais ya label hiyo, Diamond Platnumz, ameiambia Bongo5 kuwa ataimba Mchiriku, Hip Hop na muziki wowote ilimradi apate pesa.

“Mashabiki wangu wategemee vitu vizuri mimi naimba, nachana, nitaimba Singeli, Mchiriku na nitaimba kila style nikiwa WCB ilimradi nipate pesa ya kula na maisha yaende na mashabiki wangu pia wapende kitu nachokifanya, kwa hiyo sitawaangusha nitakuja vizuri,” alisema Queen Darleen.

Aliongeza, “Watu wanajua uongozi wa WCB haukoseagi kwenye kazi, mimi naimani wao ndo wanajua Queen Darleen aje kwa mtindo gani kwa sababu mimi nitafanya kila aina ya muziki, wao wataangalia nini kitoke,”

Muimbaji huyo ni msanii wanne kutangazwa kusaini ndani ya label ya WCB baada ya Harmonize, Raymond pamoja na Rich Mavoko.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents