Burudani

Dayna Nyange adai mastaa wanaotoka na wasanii wenye umri mdogo wengi hufuata mkumbo

Hitmaker wa ‘Angejua’, Dayna Nyange amedai kuwa mapenzi ya mastaa wengi wanaotoka na wasanii wenye umri mdogo yamekuwa kama fashion siku hizi huku wengi wao wamekuwa wakifuata mkumbo.

Dayna

Akiongea na Bongo5, Dayna amesema, “Imekuwa kama fashion sasa hivi na wengine wamekuwa wanakwambia ni mapenzi tu.”

“Sawa kuna mapenzi lakini wengi wao wamekuwa wakifuata mikumbo. Siyo kama wanaume wa rika lao wanakuwa hawapo, wapo lakini wanaamua tu kufanya hivyo,” alisema Dayna.

“Wakati mwingine ujana na ustaa unaweza ukafanya kitu ambacho siyo kama ulitaka kufanya ila kwa sababu ulishaona kama ukifanya mashabiki watapenda. Binafsi mimi sifikirii wala sitoweza wala kutamani kudate na mtu nimemzidi umri,” aliongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents