Burudani

Staa wa Hollywood auawa na gari yake mwenyewe iliyorudi reverse na kumgonga

Siku yako ikifika imefika. Muigizaji wa filamu ya Star Trek, Anton Yelchin ameuawa na gari yake mwenyewe.

475521698

Mwili wa Yelchin ulibanwa kwa nguvu kwenye geti la nyumba yake. Staa huyo alikuwa anatoka kwenye nyumba yake lakini baadaye alishuka na kuiacha gari kwenye neutral.

35773B2F00000578-3649368-image-a-41_1466369009882
Mwili wake ulikuwa ukiwa umebanwa na gari yake upande huo wa kushoto wa geti

Gari yake Jeep Grand Cherokee ilianza kurudi nyuma na kumkandamiza kwenye geti la chuma la nyumba yake. Muigizaji huyo alitakiwa kwenda kwenye mazoezi usiku wa Jumapili lakini marafiki zake walipatwa na wasiwasi baada ya kuona hajatokea na ndipo walipoamua kwenda nyumbani na kumkuta akiwa amegongwa na kubanwa kwenye geti huku gari yake ikiwa imewakwa.

3575A15000000578-3649368-image-m-24_1466360061971

Alitangazwa kuwa amekufa hapo hapo.

Kulikuwa na kamera za usalama kwenye nyumba yake ambayo inaweza ikawa imelichukua tukio zima.
Muigizaji huyo mzaliwa wa Urusi alikuwa akiishi Studio City, California.

Polisi wanachunguza kifo hicho cha ghafla hapo hakuna dalili zozote za kuwepo hila.

‘It appears he momentarily exited his car and it rolled backward, causing trauma that led to his death,’ msemaji wa LAPD Jenny Houser aliiambia tovuti ya The Hollywood Reporter.

Msemaji wa Yelchin alithibitisha kifo chake kwa maelezo: Anton Yelchin was killed in a fatal traffic collision early this morning. His family requests you respect their privacy at this time‎.’

Amewahi kuigiza pia kwenye filamu ya Terminator Salvation, Only Lovers Left Alive NA Hearts In Atlantis.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents