Burudani

R. Kelly akimbizwa hospitalini baada ya kuanguka, wakati akitazama makala ya namna alivyowafanyia vitendo vibaya mabinti wadogo

Kwa mujibu wa mtandao wa Hot97 umeripoti kuwa mwanamuziki mkogwe R Kelly amekimbizwa hospital hii ni baada ya kupata tatizo la kuanguka mara kwa mara wakati alipokuwa akitazama Makala ya Life Time.

inayoonyesha namna ambavyo msanii huyo alivyokuwa akiwafanyia vitendo vya unyanyasaji wa kingono wanawake waliokuwa na umri chini ya miaka 18.

Imeripotiwa kuwa Kellz alipata shambulio la hofu (panic) na kuathiri afya yake siku moja kabla ya kuoneshwa rasmi filamu ya ‘Surviving RKelly’ ya kampuni ya Lifetime. Hot97 na TMZ vimeeleza kuwa mwimbaji huyo alitetereka kiafya kiasi cha kutafuta msaada wa kitabibu.

Hii ilimpelekea R.Kelly kuamua kutotumia muda wake akiwa nyumbani kwani ingemletea madhara makubwa, ndio maana ameanza kuonekana kwenye kumbi mbali mbali za starehe.

Taarifa nyingine ni kwamba polisi mjini Chicago walimuweka chini ya ulinzi Kellz jana kufuatia simu ya dharura iliyopigwa kwao ikihitaji msaada wao mara baada ya wasamaria wema kumuoana Kellz amesimama na wanawake wawili kwenye jengo la Trump Tower, baada ya kuwasili walifanikiwa kumshikilia huku wakifanya mazungumzo pembeni na wanawake hao ambao ilionekana kuwa hakuna chochote kibaya kilichokuwa kinaendelea.

Kellz aliachiwa na kuondoka, wanawake hao walitambulika kwa majina (Joycelyn Savage & Azriel Clary) ambapo inadaiwa kuwa wazazi wao waliwahi kuingia kwenye mgogoro mzito na Kellz wakidai amepita na mabinti zao wote.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents