Habari

Rais Lungu aahidi kutatua changamoto za TAZARA

Rais wa Zambia, Edgar Lungu alitembelea mamlaka ya reli Tanzania na Zambia, TAZARA, kuwahakikishia wafanyakazi kuwa Zambia itafanya jitihada zote kuhakikisha inatatua changamoto za uendeshaji.

53

Rais Lungu alikutana na Rais Dkt John Magufuli kuzungumzia mipango mbalimbali ya maendeleo na kusisistiza kuendeleza ushirikiano ulioanzishwa na waasisi wa mataifa hayo akiwemo Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Kamuzu Banda wa Zambia.

Katika ziara ya Rais Lungu ametembelea mabomba ya kusafirishia mafuta TAZAMA na kujionea shughuli za uendeshaji na baadaye kuelekea Ikulu kwaajili ya mazungumzo. Rais Lungu alikuwa nchini katika ziara yake ya kiserikali ambapo alipata mualiko kutoka kwa mwenyeji wake Rais Magufuli.

Rais Lungu aliyewasili Tanzania siku ya Jumapili, ameondoka nchini Jumanne hii.

Hizi ni baadhi ya picha:

unnamed-1-1
Rais John Magufuli akiagana na Rais Edgar Lungu katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere.

rg1a4552

rg1a4480

rg1a4518
Waziri mkuu wa Tanzania akiagana na Rais Edgar Lungu.

BY: EMMY MWAIPOPO

PICHA: OFISI YA WAZIRI MKUU

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents