Habari

Rais Magufuli aeleza alivyonusurika kifo kwa kunyweshwa sumu (+Video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt, John Pombe Magufuli amekiri kuwa alishawahi kunyweshwa sumu akiwa Jijini Dodoma kwenye utawala wa awamu ya tatu ya Mzee Benjamin Mkapa.

Akiongea leo Jumanne Novemba 12, 2019, kwenye uzinduzi wa kitabu cha ‘My Life, My Purpose’ cha Rais Mstaafu Mzee Mkapa, Rais Magufuli amesema uchapaji kazi wake uliotukuka na kupongezwa na Mzee Mkapa pale alipokuwa amefanya vizuri ndio kulisababisha baadhi ya viongozi wenzake kumchukia hadi kumuwekea sumu.

Nakumbuka Mzee Mkapa pale tulipofanya kazi vizuri, Alipata furaha sana kwa kazi nzuri za kwenye barabara,  Na baadae akatamka kuwa mimi ni askari wake wa mwavuli namba moja. Kwa kufanya kazi ya barabara vizuri. Siwezi kusahau swala hilo maishani mwangu, Kwa sababu licha ya dhamira nzuri ya Mzee Mkapa suala hilo liliniletea mimi matatizo binafsi. Nilianza kuona baadhi ya mawaziri tena wengine wa ngazi za juu kabisa wakaanza kunichukia. Na muda si mrefu baada ya hapo nikanyweshwa sumu Dodoma, Ambayo al-manusura iondoe uhai wangu, Lakini kwa neema za mwenyezi Mungu nikakiepuka kifo,“Amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amesema baada ya tukio hilo, Alimuendea Mzee Mkapa na kumuomba ajiuzulu lakini akapewa moyo aendelee kuchapa kazi na akapewa ulinzi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents