Habari

Rais Magufuli afaya uteuzi huu leo Ikulu jijini Dar Es Salaam

Rais Magufuli afaya uteuzi huu leo Ikulu jijini Dar Es Salaam

Rais Magufuli, amefanya uteuzi wa Wenyeviti watatu, watakaoongoza bodi za taasisi mbili za Serikali na Moja ya ubia na Sekta binafsi, akiwemo Gabriel P Malata kuwa Mwenyekiti na kuiwakilishi Serikali katika Bodi ya Kampuni ya Airtel, ambapo Profesa Malata ni Naibu Wakili Mkuu wa Serikali.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.

Wengine ni Profesa Martha Qorro kuwa Mwenyekiti wa Baraza Chuo Kikuu cha Mipango, ambapo Profesa Qorro ni Profesa mshiriki wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, pamoja na Profesa Joseph Rwegasira Buchweshaija, kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela.

Taarifa hiyo imetolewa leo Januari 31, 2020 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, imeleza kuwa uteuzi wa viongozi hao umeanza jana Januari 30.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents