Habari

‘Hatukubali wanafunzi ambao sisi ndiyo tunawapa mikopo, waitishie Serikali’ Naibu Waziri Wiliam Ole Nasha (+Video)

'Hatukubali wanafunzi ambao sisi ndiyo tunawapa mikopo, waitishe Serikali' Naibu Waziri Wiliam Ole Nasha (+Video)

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Wiliam Ole Nasha amesema kuwa kilichotokea siku za hivi karibuni katika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ni kurudisha mambo nyum na hizi sio zama za kuvutana na Wanafunzi kuhusiana na maswala ya mikopo kwa kuwa siku hizi fedha hizo hutolewa Miezi miwili kabla ya Chuo Kufunguliwa.

Ila kinachotokea ni michakato na changamoto za ndani ya vyuo vyenyewe na kusema kuwa hata kilichotokea katika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ilikuwa sehemu ndogo ya Wanafunzi ambao bado taarifa zao zilikuwa hazijakamilika huku Naibu Waziri Ole Nasha akisitiza kuwa hawatokubali Wanafunzi ambao wanapata mikopo kutishia Serikali.

”Hata hivyo hatutakaa tukubali, Wanafunzi ambao sisi ndiyo tunawapa mikopo kama Serikali, kutishia Serikali kwamba msipotoa fedha katika saa 72 wataandamana”

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents