Habari

Rais Magufuli aiogopa orodha ya wafungwa wanaotakiwa kunyongwa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ameomba kutopewa orodha ya wafungwa ambao wamehukumiwa kunyongwa.

Rais Magufuli amesema hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaama wakati akimuapisha Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma na kusema anatambua kuwa idadi ya wafungwa waliohukumiwa kunyongwa.

“Lakini ieleweke pia wakati namchagua Jaji Mkuu sikupata shinikizo lolote ningeweza nikakuteua wewe, ningeweza kumteua mtu yoyote kwa sababu nilikuwa na sampo kubwa lakini palikuwepo na priority zangu ambazo niliziweka lakini nilimtanguliza pia Mungu kwamba unapoteua kiongozi wa watu ambae anakuja kutoa judgement ni lazima umtangulize Mungu kazi ya ujudge mkuu ni kazi ngumu,” amesema Rais Magufuli.

“Utahukumu kunyonga kama ambavyo mmekuwa mkifanya mnapoleta kwetu sisi wanasiasa tunaogopa kuidhinisha kunyonga na naambiwa wako wengi tu ambao wamekwisha kuhukumiwa kunyongwa lakini naomba hiyo orodha wala msiniletee,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents