Habari

Rais Magufuli amtaka kiongozi huyu ajiandae kustaafu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli amemtaka Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka(DAWASA), Archard Mtalemwa ajiandae kustaafu.

Rais ameyasema hayo leo akiwa katika ziara yake ya siku tatu mkoani Pwani ambapo alizungumzia mradi wa maji na ulipaji katika taasisi zote huku akitaka umeme ukatwe bila kujali kwa mtu ambaye hata lipa bili ya maji.

Rais Magufuli alisema “Wapo wanaouliza Archard Mutalemwa atastaafu lini? Mimi nimeanza kumsikia toka sekondari. Mutalemwa jiandae kustaafu,naongea kwa lugha nzuri hapa, nikuombe tu kuwa ustaafu mapema, inawezekana Waziri wa Maji ni rafiki yako, kama ilivyo kwa mawaziri wengine, lakini nadhani huu ni wakati mzuri.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents