Habari

Rais Magufuli apiga marufuku michango mashuleni

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. John Pombe Magufuli ameendelea kukazia sera yake ya elimu bure ambapo awamu hii amepiga marufuku michango yote inayochangishwa mashuleni.

Rais Magufuli katikati kwenye picha

Rais Magufuli amesema hayo leo Jumatano Januari 17, 2018 Ikulu, jijini Dar es salaam alipokutana na  Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.

Hata hivyo, Rais Magufuli amewataka Mawaziri hao kusimamia agizo hilo kwa shule zote za Sekondari na Msingi ili kuondoa adha ya michango.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents