Habari

Rais Magufuli asikitishwa na kifo cha mwanafunzi wa NIT, Atoa agizo hili

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambi rambi kwa wanafunzi wa chuo cha Usafirishaji (NIT) na kwa familia ya mwanafunzi aliyepigwa risasi na askari polisi juzi Ijumaa, Akwilina Akwilini.

Tokeo la picha la rais magufuli rambirambi
Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Rais Magufuli amesema amepokea taarifa hizo kwa masikitiko na kutoa agizo kwa vyombo vyote vya usalama nchini Tanzania kufanya uchunguzi wa haraka ili mtu aliyefanya tukio hilo akamatwe.

Nimesikitishwa sana na kifo cha mwanafunzi Akwilina Akwilini wa Chuo cha Usafirishaji (NIT).Natoa pole kwa familia,ndugu,wanafunzi wa NIT na wote walioguswa na msiba huu.Nimeviagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria waliosababisha tukio hili,“amesema Rais Magufuli kwenye taarifa yake aliyoichapisha kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Akwilina Akwilini alipigwa risasi na jeshi la polisi Februari 16, 2018 katika eneo la Mkwajuni -Kinondoni jijini Dar es Salaam wakati jeshi la polisi likiwatawanya wafuasi wa CHADEMA ambao walikuwa wakiandamana kwenda kwa Mkurugenzi wa uchaguzi wa Kinondoni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents