Habari

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi Moshi, Lindi

Rais John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia za watu 20 waliopoteza maisha wakati wakitoka katika Ibada huko Moshi na kwa familia za watu zaidi ya 20 waliopoteza maisha kutokana na madhara ya mvua kubwa zinazonyesha Mkoani Lindi na Mikoa mingine hapa nchini.

Watu 20 waliofariki dunia Mjini Moshi, walikuwa miongoni mwa watu waliokusanyika katika viwanja vya Majengo kuhudhuria Ibada iliyoongozwa na Mtume Boniface Mwamposa, na wamefariki dunia baada ya kukanyaga mafuta ya upako. Katika tukio hili watu 16 wamejeruhiwa.

Watu wengine zaidi ya 20 wamefariki dunia Mkoani Lindi na katika Mikoa mingine hapa nchini ambayo imekumbwa na madhara yatokanayo na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents