Habari

Rais Magufuli awasamehe Makamba na Ngeleja ”Walinitukana na nikahakikisha sauti zile ni zao 100%, nimewasamehe”(+Video) 

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli hii leo siku ya Jumatano ameamua kuwasamehe Mh Januari Makamba na William Ngeleja.

Image result for rais magufuli VS jANUARI mAKAMBA

Akizungumza katika mkutano huo mkuu wa wadau wa sekta zote za ujenzi nchini Rais Magufuli amesema siku za hivi karibuni wapo watu ambao walimtukana wakiwemo Mh Januari Makamba na William Ngeleja lakini amewasamehe.

“Nakumbuka siku za hivi karibuni kunawatu fulani walinitukana na nikahakikisha sauti zile ni zao kwao kwa zaidi ya asilimia 100.” – Rais Magufuli

Rais Dkt John Magufuli ameongeza “Nimewasamehe Mh Januari Makamba na Ngeleja, waliomba msamaha wakanigusa, nikasema hawa ni vijana wamekosea na wamekiri makosa yao, niliwasamehe na kusahau.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents