Habari
Rais Tshisekedi awasamehe waliopanga njama za kumuua Rais Laurent Kabila
Rais Felix Tshisekedi ametoa msamaha kwa watu 26 waliokuwa wamefungwa jela kwa kupanga njama ya mauaji ya Rais wa zamani wa Nchi hiyo, Laurent Kabila mwaka 2001.
Watu hao walihukumiwa vifo na kwa mujibu wa Mamlaka, baadhi yao wamefariki wakiwa gerezani, lakini hakuna hata mmoja ambaye amenyongwa.
Rais Laurent Kabila aliuawa kwa kupigwa risasi na Mlinzi wake Januari 16, 2001 na muda mchache baadaye, Mlinzi huyo alipigwa risasi.