HabariMichezo

Rais wa FIFA, Gianni Infantino awapongeza Yanga kwa Ubingwa 2021/22

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), Gianni Infantino ametuma salamu za pongezi kwa Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC 2021/22 Klabu ya Young Africans.

Infantino amesema Ubingwa huo usingewezekana bila bidii ya timu nzima, ari na kujitolea.

Amesema kila mmoja kwenye Klabu anapaswa kujivunia na kutoa pongezi kwa wote waliohusika katika mafanikio hayo.

Aidha amemshukuru rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia kwa mchango mkubwa anaoutoa katika maendeleo na ustawi wa soka la Tanzania na Kanda ya Afrika Mashariki na Kati.

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents