Michezo

Rasmi: Mrithi wa Lwandamina Yanga ni Zahera Mwinyi ‘Mkongoman’ 

Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Yanga, huwenda ikamtambulisha rasmi kocha wake, Zahera Mwinyi ‘Mkongoman’ siku chache kabla ya kuwakabili watani wao wa jadi Simba SC Aprili 29 kwenye dimba la uwanja wa Taifa.

Mwinyi mwenye uraia wa nchi mbili Ufaransa na DR Congo anarithi mikoba iliyoachwa na aliyekuwa Kocha Mkuu wa klabu ya hiyo, George Lwandamina.

Kocha huyo mwenye sifa ya upole na asiyependa kuzungumza sana amewasili jana usiku huku kwamara yake ya kwanza kutua nchini alikuwa na benchi la ufundi la DR Congo na kupokea kipigo cha  mabao 2 – 1 kutoka kwa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars mchezo wa kirafiki.

Kocha huyo alikuwa akiitajika na Yanga kwa mara kadhaa, amesema kuwa amekuja kufanya mazungumzo ya mwisho na wanajangwani hao huku akisema kuwa hapo awali ilikuwa ngumu kufuatia kuwa na mkataba na chama cha soka cha DR  Congo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents