Michezo

RASMI: Nafasi ya Zahera yachukuliwa na Mbelgiji, Yanga 

Mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu soka Tanzania Bara Young Africans wanatarajia kumpa kazi ukocha Mbelgiji, Luc Eymael ambaye anarithi mikoba ya Mkongo Mwinyi Zahera.

Luc Eymael mwenye umri wa miaka 60, ataifundisha Yanga SC ambayo ipo chini ya kocha wa muda Charles Boniface Mkwasa huku.

Tayari Yanga imemkaribisha Mbelgiji huyo kwa kuandika ujumbe wa ”Welcome to Tanzania ,welcome to Young Africans Sc, Luc Eymael from Belgium.”

Kocha, Luc Eymael kabla ya kuifundisha Yanga SC

Kazi yake ya mwisho kabla ya kutua Yanga, kocha Luc Eymael ametoka kuifundisha klabu ya Black Leopards kutoka nchini Afrika Kusini mwaka jana 2019.

Msimu wa mwaka 2018/19 mwalimu, Luc Eymael alikuwa akiifundisha timu ya Tala’ea El Gaish Sporting Club kutoka Misri. Wakati msimu wa 2017/18 akiifundisha klabu ya Free State Stars ya Afrika Kusini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents