Burudani

Ray C aeleza ya moyoni baada ya kudaiwa ameonekana kwenye chimbo la madawa ya kulevya

Rehema Chalamila aka Ray C amechukia baada ya gazeti moja la udaku nchini kuandika habari inayodai kuwa hivi karibuni alionekana akiwa katika eneo ambalo linadaiwa huwa yanapatikana madawa ya kulevya.
Ray C

Kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika: Seriously kwa kweli huwa naumia sana sana kuona binadamu mwezangu anadiriki kuniharibia jina langu ili yeye apate kula!. Hamjui mnaniathiri kiasi gani na hizi habari zenu?. Hivi unadirikije kuandika ‘usengwile’ kama huu bila hata aibu wala picha ya kuisapoti hiyo habari yani ni ujinga ujinga tu umeunganishwa na picha yangu bila hata uoga mmeichukua kutoka kwenye page yangu ya insta basi tayari mmeshapata story ili mradi tu mniharibie maisha yangu ili nyie mpate pesa mi nife maskini!!!.

Kama kweli mnauhakika na mlichoandika kwanini hamkuweka picha yangu nikivuta hayo maunga badala yake mnaweka picha ya kituo cha mkunguni ambapo madaladala husimamisha kituoni hapo. Mmepiga picha ya kituo cha mkunguni mkaona haitoshi mkaingia kwenye page yangu ya insta na kuchukua picha yangu niliojipiga mwenyewe ndio mnazitumia kunichafulia jina langu tena wakati ndio kwanza nahangaika kurudi tena kwenye kazi yangu.

Haki ya mungu sijawahi kusikia hata siku moja nyie global mmeandika kuhuau foundation yangu na mambo mazuri iliofanya japo mnajua kama mpaka sasa nimeshatoa vijana zaidi ya sabini kwenye madawa na wako fit wanatumia methadone je mnajua hilo?. Hata siju moja sikawahi pata msaada wowote kutoka kwenu japo kunichangia nauli tu ya kuja kwenye dawa kila siku hakuna hata anaenisaidia huu mwaka wa tatu bado naendelea kunywa dawa na ni kila siku ya mungu siku saba kwa wiki hakuna sikukuu wala msiba na ukikosa mwili unauma vibaya sana yani it’s not easy but am a fucking hard working woman na ni mwanamke jasiri napambana na siogopi kujaribu,naparangana na haya madawa na nayapinga na kamwe sintorudi nyuma na hizi nuksi mzipeleke kwenye familia zenu, wewe shigongo unamkosea sana mungu!. Unajifanya mlokole lakini kazi yako ni kuharibia maisha ya wenzio unasahau kuwa malipo ni hapahapa duniani!. Mimi ni kapuku tu sina mbele wala nyuma mbele yako lakini bado unanichimbia kaburi angali mi mzima. Na wewe?

Mayasa Marwata ni mpuuzi usie jua kazi yako!. Nimeisoma stori yako nimegundua ni mvivu wa kufatilia habari! eti chimbo la unga langu lajulikana sasa kama ushalijua mbona haukunipiga nikivuta huo unga unaenda kupiga picha kituo cha daladala bwege we!
Ntapambana na nyie MAHAKAMANI.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents