Burudani

Ray C alizwa na staili ya maisha ya Elizabeth ‘Lulu’ Michael, akiri alimsahau Mungu baada ya kupona

Msanii mkongwe wa muziki nchini Tanzania, Ray C amejikuta akilengwa na machozi baada ya kuangalia video iliyosambaa mtandaoni ikimuonesha Muigizaji wa Bongo Movie, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akicheza kwaya kanisani.

Ray C amedai kuwa video hiyo imemfanya akumbuke kipindi cha nyuma wakati alipopitia kwenye matatizo ya kuugua kwani kipindi hicho alikuwa ni mcha Mungu na alikuwa hakosi kanisani tofauti na sasa.

Lulu nimeangalia hii video zaid ya mara kumi nahisi!mpaka machozi yamenilenga kwakweli!Sikumbuki lini nimeingia kanisani!“ameandika Ray C kwa kujutia kwenye ukurasa wake wa Instagram na kusisitiza kuwa amejifunza jambo kutoka kwenye video hiyo.

Najiona mzima sasa na nasahau kuwa Mungu ni mkali! nimejifunza kitu kutoka kwako my dear! kikubwa sana. You Inspire Me..“amemaliza hivyo Ray C.

Picha na video ya Lulu ikimuonesha mwenye afya nzuri akiwa Kanisani akicheza na waumini wenzake ilisambaa Jumatatu ya wiki hii. Tazama video yenyewe hapa chini ikimuonesha Lulu akicheza kanisani

https://youtu.be/gJ8j8mIRen4

 

Related Articles

2 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents