Burudani

Video: Diamond kusafiri na Wema kwenda SA kwenye Birthday Party ya Tiffah

Kwa sasa sherehe ambayo inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa burudani nchini Tanzania ni Birthday Party ya Tiffah, mtoto wa rais wa WCB, Diamond Platnumz itakayofanyika nchini Afrika Kusini August 6, 2018.

Diamond kupitia uongozi wake, Jumatano hii ametangaza kusafiri na Wema Sepetu ambaye alikuwa mwanakamati katika sherehe ya arobaini ya mtoto wa Zamaradi, King Salah.

WCB wamesema wataisafirisha kamati hiyo kwa kuwa wameipenda na wanaona ni jambo zuri kwenda kushiriki nao kwenye shughuli hiyo. Mastaa wengine ambao wanaunda kamati hiyo ni Shamsa Ford, Shilole, Irene Paul, Irene Uwoya, Lamata, Kajala Masanja pamoja na wengine wengi.

Malkia wa filamu Wema Sepetu amedai wao kama wanakamati wamefurahi nafasi hiyo kwaajili ya kwenda kushiriki na Diamond katika birthday party ya mtoto huyo.

Related Articles

One Comment

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents