RC Makala atangaza hatari eneo la Kunduchi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makala amelitangaza eneo la Kunduchi lenye Volcano ya Tope kuwa eneo la hatari na halifai kwa makazi na kuwataka Wananchi wa familia Tisa ambazo makazi yao yameathiriwa kuanza kuchukuwa tahadhari.

RC Makala akizungumza jambo na baadhi ya wananchi wa eneo la Kunduchi

RC Makala amesema hayo alipotembelea na kukagua eneo hilo kujionea athari za Volcano hiyo na kulielekeza Jeshi la Polisi kuweka uangalizi Katika eneo hilo.

Aidha Mh.  Makala amesema taarifa ya kitaalamu iliyowasilishwa ofisini kwake inaeleza kuwa eneo hilo halifai kwa makazi ndio maana amefika kuwataka kuchukuwa tahadhari wakati Serikali inaangalia hatua za kuchukuwa.

Pamoja na hayo ameelekeza eneo hilo kuwekewa alama za tahadhari ili kuwaepusha wananchi na maafa.

Related Articles

Back to top button