RC Makalla azuia watu kuishi eneo la Volcano Kunduchi (+ Video)

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, amelitangaza eneo la Kunduchi lenye Volcano ya tope kuwa ni eneo la hatari na halifai kwa makazi na kuwataka wananchi wa familia 9 ambazo makazi yao yameathiriwa kuanza kuchukuwa tahadhari.

RC Makalla amesema hayo alipotembelea na kukagua eneo hilo na kujionea athari za Volcano hiyo na kulielekeza Jeshi la Polisi kuweka uangalizi katika eneo hilo.

Aidha, RC Makalla amesema taarifa ya kitaalamu iliyowasilishwa ofisini kwake inaeleza kuwa eneo hilo halifai kwa makazi ndio maana amefika kuwataka kuchukuwa tahadhari wakati serikali inaangalia hatua za kuchukua.

Pamoja na hayo RC Makalla ameelekeza eneo hilo kuwekewa alama za tahadhari ili kuwaepusha wananchi na maafa.

Related Articles

Back to top button