Michezo

Rekodi ya dunia yampeleka Neymar PSG

Mchezaji wa timu ya taifa ya Brazili na klabu ya Barcelona ya nchini Hispania, Neymar da Silva Santos Junior amekubali dili la kujiunga na matajiri wa Ufaransa Paris Saint-Germain kwa dau nono la pauni milioni 195.

Mchezaji wa timu ya taifa ya Brazili na klabu ya Barcelona ya nchini Hispania, Neymar da Silva Santos Junior

Kwa mujibu wa Esporte Interativo kablu ya PSG ilikiambia chombo cha habari cha L’Equipe kwamba mchezaji huyo aliulizia juu ya daulake hilo na hivyo kutoa ishara kuwa mipango inakwenda vizuri.

Chombo cha habari za michezo cha Esporte Interativo kutoka nchini Brazili kimeeleza kuwa star huyo wa Barcelona usajili wake wa pauni milioni 195 kwenda PSG utaweka rekodi ya duni.

Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona, Robert Fernandez  ameeleza kuwa mkataba wa mchezaji huyo na Barcelona unakifungu kinachoeleza klabu yoyote itakayo hitaji huduma yake italazimika kutoa kitita cha pauni milioni 195.

By Hamza fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents