Burudani

Rich Mavoko kutumbuiza Burundi kesho, awaondoa hofu mashabiki

Msanii wa muziki anayetamba na wimbo ‘Pacha Wangu’, Rich Mavoko amewatoa hofu mashabiki wa muziki nchini Burundi kwa kusema kuwa ratiba ya show yake nchini humo ipo kama ilivyopangwa ambapo kesho anapanda ndege na kuelekea nchini humo.

Rich Mavoko

Kituo cha redio cha Rema FM cha Burundi, kimedai kuwa msanii huyo alikuwa aende nchini humo Alhamis hii lakini baada ya msanii huyo kuonekana akiwa nchini Uganda kumsupport Jose Chameleone kwenye show yake ya Serena Hotel, aliwaacha njia panda mashabiki wa Burundi.

Akizungumza na Bongo5 leo akiwa nchini Uganda, Rich Mavoko amesema ratiba yake ipo kama kawaida Ijumaa hii atasafiri kwa ndege mpaka nchini Burundi.

“Asubuhi ya kesho ndo naelekea Burundi na ndege ya asubuhi na kwenye saa 4 nitakuwa nimeshafika,” amesema. “Ratiba yangu ilikuwa ni kesho na show itakuwa tarehe 20, Uganda sio mbali ni hapa tu. Nimekuja kumsupport kaka yangu Jose Chameleone na baada ya hapo ndo safari ya Burundi itaanza. Kwahiyo wasiwe na wasiwasi kila kitu kipo sawa.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents